Mradi wa Kujenga Ujuzi kwa Maendeleo na Uingiliano wa Kikanda katika Afrika Mashariki (EASTRIP) imetoa zaidi ya Shilingi bilioni 37 kwa Chuo cha Ufundi Arusha

Published on Saturday 14 August, 2021 14:46:20

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi kwa Maendeleo na Uingiliano wa Kikanda katika Afrika Mashariki (EASTRIP) imetoa zaidi ya Shilingi bilioni 37 kwa Chuo cha Ufundi Arusha kwa ajili ya kuimarisha Kituo cha Mafunzo na Utafiti wa Nishati Jadidifu cha Kikuletwa (KRETC) ili kukifanya kuwa kituo mahiri cha uzalishaji wa nishati jadidifu.?
?
Akizungumza na waandishi wa habari walio kwenye ziara ya kutembelea miradi ya Elimu iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji wa Mradi wa EASTRIP Kituo cha Kikuletwa Dkt. Erick Mgaya amesema fedha hizo ni mkopo wa Benki ya Dunia wenye lengo la kuandaa nguvu kazi ya kutekeleza na kusimamia miradi ya kikanda yenye mikakati ya kimaendeleo iliyomo ndani ya \afrika Mashariki.?
?
Dkt. Mgaya ameendelea kuelezea kuwa Kituo hicho cha Mafunzo na Utafiti cha Kikuletwa ni miongoni mwa vituo vinne nchini ambavyo vimewezeshwa kuwa vituo mahiri vya mfano vya kutoa mafunzo ya elimu ya ufundi ambapo Kituo cha Kukiletwa kitazalisha Umeme kwa kutumia nguvu za maji, mionzi ya Jua, Upepo, Tungamo taka pamoja na kujenga mitambo? itakayowezesha kuzalisha umeme wa nguvu za maji wa 1.65 MW.?
?
“Uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati?ya maji katika ukanda wa Afrika Mashariki?hakuna chuo ambacho kinatoa mafunzo kwa nadharia na? kwa vitendo kwa pamoja hivyo Kituo kitajenga mitambo ya uzalishaji wa umeme kwa nguvu za maji wa 1.65MW na kuwezesha mafunzo ya kitaalamu yanafanyika hapa, ambapo mpaka sasa tuna mkataba na TANESCO wa kuwajengea uwezo watumishi wake”. amesema Dkt. Mgaya?
?
Aliongeza kuwa kupitia fedha hizo Kituo kitajenga maabara mbili, mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kila moja, karakana sita,? jengo la utawala, madarasa, kumbi za mihadhara, bwalo la chakula, kituo cha afya na nyumba za watumishi kwa ajili ya kufundishia?na kukiwezesha kufanya kazi katika mazingira rafiki na kuongeza udahili kufika wanafunzi 643?ukilinganisha na idadi iliyopo sasa ambao ni 168. ?
?
Awali Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha? \Dkt. Yusuph Mhando aliwaambia waandishi wa habari kuwa Mradi wa EASTRIP katika chuo hicho unalenga kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Kikanda katika Nishati Jadidifu ambapo tayari Chuo kimeshapokea Shilingi bilioni 11.2 ambayo ni asilimia 30ya fedha yote ya mradi.?

Read 887 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top