BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUFADHILI MIRADI YA ELIMU NCHINI

Published on Saturday 04 September, 2021 22:56:40

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameishukuru Benki ya dunia kwa kuendelea kufadhili miradi ya elimu nchini ambayo imesaidia kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu na kuongeza Ubora.

Waziri Ndalichako amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi Mara Warwick kwa lengo la kupitia taarifa ya tathmini ya miradi ambayo inatekelezwa kwa ufadhili wa benki ya Dunia katika Sekta ya Elimu nchini, kuainisha changamoto pamoja na kujua malengo ya mbele ya elimu ili kuhakikisha elimu inatoa mchango stahiki katika kuleta maendeleo na kujenga uchumi wa nchi.

Waziri Ndalichako ameelezea baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa Mradi wa Lipa kulingana na Matokeo ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia kuwa ni kujenga Vyumba vya madarasa 10,409, matundu ya vyoo 20,507 mabweni 646, nyumba za walimu 91, majengo ya utawala 37, maktaba 49, maabara 29 na shule mpya 44.

Mradi umewezesha, kuimarisha mifumo ya kuchakata takwimu kwenye sekta ya elimu ambapo kwa sasa takwimu zinakusanywa moja kwa moja kutoka shuleni jambo ambalo limeongeza ufanisi katika kupata takwimu za elimu kwa usahihi. Aidha mradi pia umewezesha kuimarisha uwiano kati ya kitabu na wanafunzi.

“Kwa kweli ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo na nchi marafiki, matunda yake tunayaona hasa watoto wa kitanzania wanapopata elimu bora, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii li kuhakikisha kwa pamoja tunaleta maendeleo kwa watanzania,” amesema Prof. Ndalichako.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi Mara Warwick amesema wapo tayari kuendelea kufadhili miradi ya elimu ili kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora na kuipongeza Serikali kwa kutimiza vigezo vilivyowezesha vya Mradi wa Elimu ya Juu kwa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) kuanza utekelezaji.

Read 2079 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top