Katibu Mkuu wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi, leo amekabidhi eneo la kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania ili wakala hao waandae mpango wa matumizi ya eneo hilo kwenye makao makuu ya nchi mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Tarishi ameelekeza kuwa eneo hilo ni maalumu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zitakazotumiwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kama vile Mamlaka ya Elimu Tanzania, -TEA, Bodi ya Mikopo -HESLB, na Tume ya Vyuo Vikuu nchini -TCU.
Katibu Mkuu Tarishi ameiagiza TBA kuandaa Michoro ( Design) na Kufanya ujenzi wa majengo ya Ofisi za wizara hiyo ujenzi ambao utafanyika Kwa Awamu.
TBA imesisitizwa kukamilisha ujenzi mapema iwezekanavyo Kwa mujibu wa makubaliano.