Jumatano, 15 Novemba 2017 04:22

TAARIFA KWA UMMA :TAMKO LA NAIBU WAZIRI KUHUSU TSSF

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa William Tate Ole Nasha amesimamisha mara moja shughuli za utoaji mikopo zilizokuwa zinafanywa na Taasisi ya Tanzania Social Support Foundation (TSSF). Hatua hiyo imefikiwa baada ya Wizara kujiridhisha kuwa vitendo  vilivyokuwa vinafanywa na  taasisi hiyo ni kinyume na sheria, vilevile taasisi imeudanganya umma kuwa ina uwezo wa kutoa mikopo jambo ambalo siyo la kweli.

Naibu Waziri ameyasema hayo mara baada ya kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Donati Silla na Katibu Tawala wake Bw. Marwa Chacha kwa lengo la kuchambua nyaraka mbalimbali za Tasisi hiyo. Katika uchambuzi huo imebainika kuwa mchakato wote uliokuwa unafanywa na Taasisi hiyo ni wa kilaghai kwa lengo la kuwahadaa wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu.

Katika uchambuzi huo imebainika kwamba Taasisi hiyo haina uwezo wa kifedha wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu. Katika mahojiano na viongozi hao imebainika kwamba jumla wa wanafunzi 198 tayari wamerubuniwa na kujiunga na mpango wa mikopo wa taasisi hiyo.

Naibu Waziri Ole Nasha ameelekeza kusitishwa kwa akaunti zote ambazo zimekuwa zikitumika kufanya miamala mbalimbali ya fedha. Akaunti hizo zinasemekana kuwa zimefunguliwa katika Benki za CRDB, NMB, na EXIM.

Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri ameviagiza vyuo vyote vya Elimu ya juu kutopokea wanafunzi kwa barua zinatoka TSSF, na kuwa Wizara itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wanafunzi 198 ambao tayari wako vyuoni na waliahidiwa kupatiwa mikopo na taasisi hiyo.

Tayari watuhumiwa akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Donati Silla na Katibu Tawala wake Bw. Marwa chacha  wanashikiliwa na Jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

Imetolewa na;

Mwasu Sware

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

14, Novemba 2017.

Read 33682 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…