Jumatatu, 09 Oktoba 2017 07:25

NDALICHAKO: SERIKALI INA FEDHA ZA KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU.

Serikali imeahidi kutoa kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa maabara nzuri na ya kisasa ya kemia kwa ajili ya Chuo kikuu kushiriki cha Elimu Mkwawa kilichopo mkoani Iringa.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako mara  baada ya kutembelea na kujionea hali ya miundombinu chuoni hapo  na kuahidi kuwa fedha hizo za ujenzi  zitakuwa zimepatikana hadi ifikapo Desemba mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo.

Akiwa chuoni hapo Waziri Ndalichako  ameshuhudia ujenzi unaoendela wa jengo la mihadhara ambalo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1200 kwa wakati mmoja.

Waziri  Ndalichako amewataka wanafunzi wa kitanzania kutumia fursa ya ufadhili iliyotolewa na nchi ya Hungary kwa wanafunzi 90 katika kipindi cha miaka mitatu  kuhakikisha wanajipanga vizuri ili waweze kufanya mitihani kwa weledi na  ili waweze kufanikiwa kupata ufadhili huo.

 "Kwa kipindi cha miaka 3 Tanzania tumepata ufadhili wa kwenda kusoma Hungary,  ufadhili huo siyo kwamba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia watakuwa wanachagua wanafunzi, bali wanafunzi watapatikana kwa ushindani kwa kufanya mitihani vizuri kwenye masomo wanayokwenda kusoma pamoja na   na lugha ndiyo watachaguliwa", alisema Profesa Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema kwa kutambua umuhimu wa Rasilimali watu wenye sifa zinazotakiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika bajeti yake kwa  mwaka wa fedha 2017/ 2018 imetenga kiasi cha bilioni 2 kwa ajili ya ufadhili wa walimu  wa vyuo vikuu kwa ajili ya kwenda kujiendeleza ndani na nje ya nchi. 

Pia Waziri Ndalichako amekagua  ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo katika shule ya Msingi ya kalenga, ujenzi huo umetekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia programu ya Lipa kulingana na matokeo. (P4R).

Imetolewa na; 

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

7/10/ 2017

Read 5750 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…