Alhamisi, 05 Oktoba 2017 07:13

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MENEJIMENTI YA VETA.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Mamlaka ya Elimu, na Mafunzo ya Ufundi Stadi -Veta -kurejesha haraka fedha ambazo ni masurufu  kiasi cha shilingi Milioni 600 ambazo hazionekani kwenye kumbukumbu na wala hazina maelezo kuwa zimetumikaje.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo mkoani Dodoma wakati akizungumza na menejimenti ya Taasisi hiyo mkoani Dodoma ambapo amewataka wale wote waliohusika na kutumia fedha hizo wazirejeshe na ziweze kufanya kazi iliyokusidiwa vinginevyo fedha hizo zikatwe kwenye mishahara yao.

Waziri Ndalichako amesema haridhishwi na uwajibikaji wa Taasisi hiyo kutokana na   kushindwa kusimamia shughuli za utekelezaji na badala kufanya kazi kwa mazoea.

Waziri Ndalichako ameitaka VETA kuhakikisha inafanya uhakiki wa vyeti kwa kuwa hayo ni maagizo ya   Serikali kwa nchi nzima, pia ameelekeza kama zipo taasisi zilizochini ya Wizara yake na hazijafanya uhakiki zifanye haraka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya  Taasisi hiyo  Peter Maduki amezungumzia suala la uwajibikaji na utendaji kazi ambapo menejimenti imekubaliana kuwa dhana ya ugatuwaji iimarishwe ambapo wamekubaliana kuwa watasambaza waraka ili watumishi wa Taasisi hiyo wausome  na kutoa maoni kwa lengo la kuboresha hadi ifikapo Novemba 30, 2017.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Read 4723 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…