Jumatano, 20 Septemba 2017 13:57

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI.

Nafasi za kazi kwa walimu wa shule za msingi bado zipo. Hivyo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inakaribisha maombi ya kazi kwa walimu waliohitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti (IIIA) mwaka 2014/15.

 

Waombaji waliohitimu katika mwaka wa masomo 2014/15 ambao walituma barua za maombi kwa Tangazo la nafasi za kazi la tarehe 10/08/2017 hawatakiwi kutuma maombi tena kwa kuwa barua zao zimepokelewa.

Hivyo, Tangazo hili linawahusu walimu wa Cheti (Astashahada) ambao hawakutuma maombi ya kazi kutokana na kutotajwa kwenye Tangazo la ajira lililopita.

Sifa za waombaji - walimu wa shule za Msingi

 1. Astashahada ya Ualimu iliyotolewa na chuo kinachotambuliwa na Serikali.
 2. Cheti cha Kidato cha 4.
 3. Wahitimu wenye cheti cha Kidato cha 6 watapewa kipaumbele.

Utaratibu wa kutuma Maombi

 1.  Maombi yatumwe kupitia Posta kwa njia ya Rejesta (EMS). Juu ya bahasha iandikwe kwa mkono “Maombi ya kazi ya Ualimu – Msingi”.
 2.  Mwombaji aambatishe nakala za vyeti vilivyothibitishwa (Certified) na Mwanasheria pamoja na “Results slip”.

 

TANBIHI:      Barua za maombi zisiwasilishwe kwa mkono. Barua zitakazo wasilishwa kwa mkono hazitapokelewa.

Masuala mengine ya kuzingatia

 1. Mwombaji aandike majina yake yote matatu. Kama vyeti vina majina mawili, utaratibu wa kisheria wa kuongeza jina uzingatiwe.
 2. Mwombaji aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
 3. Mwombaji aandike namba ya simu na baruapepe kama anayo.
 4. Mwisho wa kupokelewa maombi ni tarehe 4/10/2017.

Maombi yatumwe kwa:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,

S.L.P 10,

40479 DODOMA.

 

Imetolewa na:

KATIBU MKUU

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

20/09/2017

Read 25580 times

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: Block 10
 •               College of Business Studies and Law
 •               University of Dodoma (UDOM)
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…