Ijumaa, 16 Juni 2017 16:16

MAAMISHO YA KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.

Mkurugenzi wa Elimu ya juu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Sylivia Temu akizugumza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa Afrika, ambapo amewaasa wazazi na walimu kuwafundisha wanafunzi na watoto maadili yaliyo mema. Maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Humekwa, kilichopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Mkurugenzi wa Elimu ya juu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Sylivia Temu akizugumza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa Afrika, ambapo amewaasa wazazi na walimu kuwafundisha wanafunzi na watoto maadili yaliyo mema. Maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Humekwa, kilichopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Sylivia Temu amewataka Wazazi, walezi na walimu  kuwalea watoto  katika misingi ambayo itawafanya wawe na maadili mema ili waje kuwa viongozi, na  wazazi bora katika maisha yao ya baadae.
 
Profesa Temu amesema hayo hii leo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mtotot wa Afrika ambayo yamefanyika kwenye kijiji cha Humekwa, Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
 
Profesa Temu amesewasihi Watoto kupenda kusoma na kuacha kujiingiza kwenye makundi ya matumizi ya  dawa za kulevya, na badala yake watoto wajikite zaidi katika kusoma kwa bidii ili wawe  viongozi bora na wenye maadili sahihi katika taifa letu.
 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya  siku ya mtoto wa Afrika ni: Maendeleo Endelevu 2030 " Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto."
 
Maadhimisho hayo ambayo kufanyika kila mwaka juni 16 yameadhimishwa kwenye mikoa mbalimbali nchini kote.

 

Read 1718 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…