Jumanne, 13 Juni 2017 13:08

KILELE CHA SIKU YA ELIMU

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wageni mbalimbali ambao hawapo pichani katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Elimu ambapo amesisitiza zaidi suala la wanafunzi kusoma kwa bidii na kudumisha nidhamu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanafunzi nchini kuwa na Nidhamu kwani bila nidhamu hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana.
 
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo hii leo mjini Dodoma wakati akikabidhi tuzo na zawadi mbalibali kwa  wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kumaliza shule ya msingi, kidato cha Nne na wale wa kidato cha sita ambapo amewasisitiza wanafunzi wa kike  kujiepusheni na mapenzi wakati wakiwa mashuleni.
 
Waziri Ndalichako amewataka wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidii, ambapo pia  amewaonya wanaowanyemelea wanafunzi kwa lengo la kuwaharibia masomo na ndoto walizonazo  kuwa  sheria ni kali na  ikithibitika  muhusika atakwenda jela miaka 30.
 
Waziri Ndalichako amesema Maadhimisho haya yanatakiwa kujenga ari na  motisha katika kuhakikisha vijana wanafanya vizuri katika masomo yao.
 
Viongozi wengine walioambata na waziri katika shughuli hiyo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo na Naibu Katibu Mkuu Profesa Saimon Msanjila.
 
Kauli mbiu ya siku ya Elimu ni: Elimu ni nguzo muhimu kwa Maendeleo ya Viwanda.
Read 1512 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…