WITO WATOLEWA KWA WADAU KUTOA MAONI MAANDALIZI YA MPANGO WA TATU WA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU

Published on Thursday 02 September, 2021 23:00:45

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo ametoa wito kwa wadau wa elimu kuendelea kutoa maoni katika hatua mbalimbali za maandalizi ya Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu ili kuongeza wigo na ubora wa elimu inayotolewa kwa Watanzania.

 Wito huo, ameutoa Jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya sekta ya elimu wakati wakijadili taarifa ya uchambuzi wa hali halisi ya sekta ya elimu kwa mustakabali wa  uimarishaji wa Sekta.

Amesema Wizara ipo katika uandaaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (2021/22 - 2025/26), hivyo ni vizuri kufanya uchambuzi wa hali halisi ya sekta katika kipindi cha utekelezaji wa mpango uliomalizika ili kujua yale yaliyopangwa yamefanikiwa kwa kiasi gani.

“Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu Awamu ya pili (2016/17 - 2020/21)  umemalizika, hivyo uandaaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (2021/22- 2025/26) umeanza na hatua ya kwanza ni kufanya tathmini ya hali halisi ya sekta katika kipindi cha utekelezaji wa mapngo uliomalizika muda wake. Kazi hiyo ya kufanya uchambuzi ndio iliyotukusanya hapa leo hivyo nawaomba mtoe mapendekezo yenu katika ya namna ya kuboresha sekta ya elimu nchini,” amesema Katibu Mkuu Akwilapo

Read 278 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top