WAZIRI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA)

Published on Monday 06 September, 2021 12:06:45

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb) leo Septemba 06, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA),  Jacqueline Mahon katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Mahon amemwelezea Waziri Ndalichako  nia ya Shirika hilo kutaka kufanya kazi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, katika  eneo la afya ya uzazi kwa kupitia Programu  inayolenga kuwalinda vijana ijulikanayo kama ‘SYP’  ambapo mazungumzo juu ya utekelezaji wa mradi huo yameanza.

Programu  ya ‘Safeguarding Young People - SYP’ itawajengea uwezo vijana, hususan wasichana, katika masuala ya makuzi na kufanya maamuzi kuhusu mustakabali wa maisha yao na itatekeoezwackwa Miaka mitatu.

Waziri Ndalichako amewataka wataalamu wa Wizara na wa UNFPA kukaa pamoja na kupitia andiko la programu hiyo ya SYP na kuishauri Menejimenti ya Wizara kuhusu utekelezaji wake na namna nzuri ya kushirikiana na UNFPA katika kuwezesha vijana kupata mafunzo.

Read 301 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top