SHULE YA SEKONDARI YA MFANO DODOMA KUKAMILIKA FEBRUARI 2022

Published on Tuesday 07 September, 2021 23:12:21

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako (Mb) Septemba 6, 2021 ametembelea Shule ya Sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu Jijini Dodoma ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo.

Shule hiyo ya bweni ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2022 itagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 17 na itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 kwa wakati mmoja.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Waziri Ndalichako amesema shule hiyo ikikamilika itakuwa na miundombinu ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia na mazingira bora ya kusomea.

"Shule hii ikikamilika itakuwa na mazingira bora ya kusomea, miundombinu ya kisasa ikiwemo viwanja vya michezo ya aina mbalimbali," amesema Waziri Ndalichako.

Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo, Kamanda wa Operesheni ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Mradi, Luteni Kanali Philemon Komanya amesema ujenzi wa shule hiyo umefikia asilimia 60 na  amemhakikishia Waziri Ndalichako kuwa kazi ya ujenzi wa shule hiyo itakamilika kwa wakati uliopangwa.

Read 2163 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top