MTANZANIA ANG'ARA TUZO ZA WANASAYANSI KIMATAIFA

Published on Sunday 19 September, 2021 17:37:29

 Katibu Mkuu wa  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad Akwilapo,  leo tarehe 20 Septemba 2021 amepokea tuzo ya Mwanasayansi Bora  katika "Plant Mutation Breeding" iliyotolewa kwa mwanasayansi mtanzania Bwana Salum Faki Hamadi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Zanzibar .

Tuzo hiyo imetolewa na Shirika la  Kimataifa la Nguvu ya Atomiki (IAEA) na kukabidhiwa Bw. Rafael Mariano Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo katika Mkutano wa  masuala ya Atomiki Duniani.unaofanyika  jijini  Viena, Austria.

Ushindi huo umetokana na   utafiti alioufanya  na kuzalisha mbegu ya mpunga inayotoa  Mavuno zaidi ya asilimia 60 ya mbegu za awali na ambayo inauwezo wa kuhimili ukame na magonjwa mbalimbali.

Read 218 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top