MADAWATI 1000 KUTOLEWA NA BENKI YA STANBIC KILA MWAKA

Published on Saturday 03 July, 2021 23:07:27

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuimarisha Sekta ya Elimu. 

Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Stanbic Madawati Initiative inayoendeshwa na Benki ya Stanbic, Waziri Nalichako alisema sekta binafsi inayo nafasi ya kushirikiana na Serikali katika kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kielimu na miundombinu  pamoja na sekta nyingine zinazogusa jamii.?
?
 
Waziri Ndalichako amesema katika kipindi cha miaka minne Serikali imejenga madarasa 11,916 kwa hiyo kuwepo na uhitaji wa madawati pamoja na miundombinu mengine.
Ndalichako ameishukuru Benki ya Stanbic kwa kuja na Kapeni hiyo ambapo atachangiwa Madawati 1000 KIla Mwaka na kuyatoa kwa shule zenye uhitaji kuanzia Meaka huu 2021. 

Ameongeza kuwa tangu kuanza kutekekezwa kwa Sera ya elimu bila malipo idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule inazidi kuongezeka na kufanya kuwa na upungufu wa miundombinu mbalimbali.?
?
“Naishukuru benki ya Stanbac kwa kuamua kuendesha kampeni hii ya kuhakikisha changamoto  ya madawati shuleni inapungua ama kumalizika kabisa, Taifa lolote haliwezi kusonga mbele bila kuwekeza katika sekta ya elimu hili ni jambo muhimu sana. Aidha naendelea kutoa wito kwa wadau wengine kuiunga mkono Serikali katika kuboresha elimu,” amesisitiza Profesa Ndalichako.?

Naye Afisa Mkuu wa Masoko katika benki ya Stanbic Desideria Mwegelo amesema kampeni hiyo inakwenda kuhakikisha inapunguza ama kuondoa kabisa changamoto ya madawati katika shule kwa kushirikiana na wadau wengine .

Kwa upande wake Mkuu wa wateja wa reja reja Omari Mtiga amesema kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya Pamoja elimubure inawezekana ina lenga kutoa madawati 1000 kila mwaka na kwamba kwa kuwa madawati hayo yanahusisha uvunaji wa miti kutengezwa basi benki hiyo itakuwa ikitoa na kupanda miti 1000  pia ili kuhakikisha mazingira yanaendelea kutunzwa.?

Read 379 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top