News (75)

Nafasi za kazi kwa walimu wa shule za msingi bado zipo. Hivyo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inakaribisha maombi ya kazi kwa walimu waliohitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti (IIIA) mwaka 2014/15.

Mwezi Juni, 2017 Wizara ilitangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa Mwaka wa Masomo 2017/18. Tangazo lilielekeza kwamba waombaji wa programu za Ualimu katika Vyuo vya Serikali waombe kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (www.nacte.go.tz). Aidha, Wizara ilielekeza kwamba waombaji wa Udahili kwenye vyuo visivyo vya Serikali, waombe moja kwa moja vyuoni.

Baada ya vyuo visivyo vya Serikali kufanya uchaguzi vilielekezwa kuwasilisha majina ya waombaji waliochaguliwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa ajili ya uhakiki wa sifa za Udahili na kisha vyuo hivyo kutangaza waliodahiliwa. Vyuo visivyo vya Serikali vitatangaza majina ya waliochaguliwa na kuhakikiwa na NACTE kuanzia tarehe 18 Septemba, 2017.

Maombi ya Udahili kwa ajili ya Mafunzo ya Ualimu katika ngazi ya Astashahada na Stashahada katika vyuo vya Serikali yalianza rasmi tarehe 10 Juni, 2017 na kuhitimishwa tarehe 20 Agosti, 2017. 

Hadi tarehe ya mwisho wa maombi,  jumla ya waombaji 15,091 (wanawake 6, 051 na wanaume 9,040) walikamilisha maombi yao. Waombaji 12,152 (sawa na 80.5%) walikuwa na sifa stahiki za kujiunga na programu za ualimu walizoziomba. Jumla ya waombaji 2,939 (19.5%) hawakuwa na sifa zinazotakiwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.

Nafasi za Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali zilizotangwa zilikuwa  ni 5,375 kwa programu ya Astashahada ya Elimu ya Ualimu na 3,731 za Stashahada mbalimbali za Elimu ya Ualimu.  Hivyo, jumla ya nafasi za Udahili kwa Mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 zilikuwa 9,106 katika vyuo 30, ambapo kati yake, vyuo 23 vinatoa Mafunzo ya Ualimu katika ngazi ya Astashahada na vyuo 16 vinatoa Mafunzo hayo katika ngazi ya Stashahada.

Uchaguzi wa waombaji ulizangatia vigezo vya jumla ambavyo ni ufaulu wa wa Daraja la I hadi la III kwa  Kidato cha Nne kwa waombaji wa Astashahada na Kidato cha Sita kwa waombaji wa Stashahada. Aidha waombaji wa Astashahada waliofaulu masomo ya Sayansi katika Kidato cha Nne walipewa kipaumbele. Ufaulu wa juu kwa waombaji waliochaguliwa kwa kozi ya Astashahada ni Daraja la I, alama 14  na kwa Stashahada ni Daraja la I, alama 6.  Ufaulu wa chini  kwa waombaji wa kozi ya Astashahada ni Daraja la III, alama 25 na kwa Stashahada ni Daraja la III, alama 17.

Kozi Ufaulu wa Juu Ufaulu wa Chini
Astashahada K4: Daraja la I, alama 14 K4: Daraja la III, alama 25
Stashahada K6: Daraja la I, alama 6 K6: Daraja la III, alama 17

Jumla ya waombaji   7,578   wamechaguliwa na hivyo kupangiwa kwa ajili ya Mafunzo ya Ualimu katika ngazi ya  Astashahada na Stashahada katika Vyuo vya Serikali vya Ualimu. Nafasi zilizobaki wazi katika vyuo vya Ualimu vya Serikali bila kujazwa ni 1,528. Hii ni kutokana na jinsi waombaji walivyofanya  uchaguzi wa vyuo. Majina ya waliochaguliwa yanapatikana katika tovuti za Wizara (www.moe.go.tz), NACTE (www.nacte.go.tz), na kwenye kurasa (profile) binafsi za waombaji na katika vyuo husika. Vyuo vya Ualimu vinatarajiwa kufunguliwa tarehe 25 Septemba, 2017. Aidha wale waliochaguliwa watajulishwa na vyuo husika juu ya utaratibu wa kufika na kuanza masomo.

Kwa kuzingatia kuwa bado kuna vyuo vyenye nafasi zilizo wazi, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) litatoa fursa ya kuwasilisha maombi kwenye programu za Astashahada na Stashahada katika fani mbalimbali nchini kuanzia tarehe  18 Septemba, 2017 hadi tarehe 1 Octoba, 2017.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kutoa wito kwa wahitimu wa Kidato cha Nne na cha Sita na wale wote walio na sifa za kujiunga na mafunzo mbalimbali kutumia fursa hiyo kufanya maombi ya Udahili. Waombaji wanashauriwa kufanya uchaguzi kwa umakini kwa kuzingatia ufaulu wao ili kuepuka kukosa nafasi kwa sababu ya kuchagua fani zenye ushindani mkubwa.

 

Taarifa hii imetolewa na katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Dr. Leonard D. Akwilapo

Supply of Textbooks and Reading Materials for 7 Zonal Teachers College Centres

Date: 28th August, 2017

  1. This Invitation for Tenders follows the General Procurement Notice (GPN) which appeared in UNDB online Issue No. AfDB34-01/15 dated20th January 2015

REQUEST FOR EXPRESSIONS OF INTEREST FOR TECHNICAL ASSISTANCE FOR CAPACITY BUILDING ON DEVELOPMENT OF DIGITAL LEARNING RESOURCES AND THE INTERGRATION OF ICT IN TEACHING AND LEARNING FOR MOEST, NACTE AND TECHNICAL INSTITUTIONS

(INDIVIDUAL CONSULTANT)

REQUEST FOR EXPRESSIONS OF INTEREST FOR CONSULTANCY SERVICES FOR CONDUCTING A SITUATIONAL ANALYSIS (LABOUR MARKET SURVEY)

REQUEST FOR EXPRESSIONS OF INTEREST FOR CONSULTANCY SERVICES FOR CONDUCTING A SITUATIONAL ANALYSIS (LABOUR MARKET SURVEY

Date 25th August, 2017

The Government of the United Republic of Tanzania has received a loan from the African Development Fund toward the cost of Support to Technical Vocational Education and Training and Teachers Education Project and intends to apply part of the agreed amount for this Loan to payments under the contract for Consultancy Services for Conducting Situational Analysis (Labour Market Survey)

Saturday, 19 August 2017 12:15

TAARIFA KWA UMMA.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuutarifu umma kuwa taarifa zinazosambaa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari

 

CONSTRUCTION OF MULTI-STOREY CLASSROOMS AND LABORATORIES BUILDING FOR ARUSHA TECHNICAL COLLEGE

Date: 17th August,2017

1.            This Invitation for Bids follows the General Procurement Notice (GPN) for this project that appeared in UNDB online with reference number AfDB34-01/15 of 20th January 2015, and on the African Development Bank Group’s Internet Website.

The Ministry of Education, Science and Technology (MoEST) has reviewed the Circular titled Application for Ministerial Approval in Respect of Foreign Experts which was issued in 2007.

Page 5 of 10

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…