Friday, 14 July 2017 16:04

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha shule

zilizotengwa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum zinapewa haki zake ikiwa ni pamoja na kupatiwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia  ili kuwezesha wanafunzi hao kupata elimu sawa na wanafunzi wengine.

Naibu Waziri Manyanya ametoa agizo hilo alipofanya ziara kwenye shule ya msingi  Sinza Maalum iliyopo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea hali ya ufundishaji na ujifunzaji katika shule hiyo, mbapo  pia amezitaka halmashauri hizo kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni yatakayosaidia kupunguza ugumu wa wanafunzi hao kuhudhuri masomo  kutokana na sababu mbalimbali za kimaumbile za watoto hao na hivyo kuwafanya wengine kushindwa kutembea umbali  mrefu kufuata shule.

Pia Naibu waziri alitembelea shule ya sekondari ya Mbweni Tete kukagua ujenzi wa madarasa, mabweni na vyoo unaofanywa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia Kupitia Programu ya lipa kulingana na matokeo, P4R kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha Tano wanaotarajiwa kuanza shule Julai 17, mwaka huu.

Read 5697 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…