Tuesday, 06 June 2017 11:19

WAZIRI MKUU AZINDUA VIFAA VYA MAABARA NA VIFAA VYA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Kassim Majaliwa amezindua usambazaji wa vifaa vya maabara na vile vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika viwanja vya jeshi lugalo, jijini Dar es salaam . 
Akizungumza katika uzinduzi huo waziri mkuu mjaliwa amesema atakayesababisha mwanafunzi kupata mimba atafungwa jela miaka 30. 
Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Wanafunzi wahakikishe wanajiilinda wenyewe kwa kuepuka vishawishi ili wafikie ndoto zao. 
Waziri mkuu Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuboresha mazingira ya Elimu hapa nchini kwa kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pia Serikali inatoa 
kipaumbele kwa wanafunzi wetu kusoma masomo ya sayansi. 
Waziri mkuu amewasihi  wazazi wawahamasishe vijana wao kusoma masomo ya Sayansi ili taifa liwe na wataalamu wa kutosha. 
Kwa upande wake waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia profesa Joyce Ndalichako amesema Shule 1696 zitapatiwa vifaa vya maabara na kati ya hizo 1625 ni shule za Kata na 71 ni shule kongwe. 
Ndalichako amesema Shilingi bilioni 16.9 zimetumika kununua vifaa vya maabara na vile vya wanafunzi wenye mahitaji maalunmu. 
Waziri Ndalichako amesema Vifaa vimekidhi mahitaji ya wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita. 
Naye waziri wa Ulinzi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) Mh. Dkt. Hussein Mwinyi amesema jeshi  liko tayari kwa kazi ya kusambaza vifaa hivyo ambapo amemuahidi waziri mkuu kuwa kazi hiyo itafanyika kwa uadilifu.
Read 5096 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…