Tuesday, 23 May 2017 13:10

VIJANA WA KIKE NA WANAWAKE VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA ELIMU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji Dkt Leonard Akwilapo leo amefungua warsha ya kuanzishwa kwa mradi wa pamoja wa uwezeshaji wa vijana wa kike na wanawake vijana kupitia elimu wenye lengo kuwatafakarisha wilaya lengwa (Ngorongoro, Kasulu, Sengerema,micheweni na mkoani pemba) juu ya vikwazo vya

elimu kwa wasichana katika maeneo yao na kubuni mikakati mbalimbali ya kukabiliana navyo ili wasichana wapate fursa ya kujiendeleza kielimu na kukuza fursa ya kuwa raia bora Zaidi.

Mradi huu wenye thamani ya dola za kimarekani milioni tano unafadhiliwa na shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea (KOICA) kupitia UNESCO ambapo unatarajiwa kuwanufaisha wasichana na wanawake vijana 8,000 walioko shuleni na wasichana 600 walio nje ya shule, kwa kuwapatia fursa ya kuimarisha ujuzi wao wa msingi, ufundi na ujuzi wa kawaida ambao utawawezesha kuwa raia bora katika nchi yao na ulimwengu kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuchangia kikamilifu katiak maendeleo ya Tanzania.

Akizungumza wakati wa ufunguzi Katibu Mkuu amesema Awamu ya kwanza ya mradi huu unalenga nchi tatu ambazo ni Tanzania, Mali na Nepal na utaratibiwa na Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na Wizara ya katiba na Sheria na kutekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni pamoja na UNFPA na UN Women.

Mradi huu ni sehemu ya mpango wa ulimwengu kupitia mashirika ya UNESCO, UNFPA na UN Women kwa ajili ya kuwawezesha wasichana kupitia elimu uliozinduliwa katika nchi sita duniani kote.

Read 4871 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…