Sunday, 07 May 2017 19:24

TAARIFA KWA UMMA: UKANUSHI VYETI FEKI.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaufahamisha umma kuwa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa baadhi ya wanataaluma wa Vyuo Vikuu vya Mzumbe, Dodoma, Dar es Salaam, Muhimbili na Ardhi pamoja na vyuo vingine ya elimu ya juu kuwa na vyeti feki sio za kweli.

 

Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako hajatoa taarifa hizo. Hivyo wananchi wanaagizwa kuzipuuza kwa kuwa hazina ukweli wowote.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa sasa yuko mkoani Arusha kushiriki katika tukio la kuaga miili ya wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent waliofariki katika ajali iliyotokea jana.

Wizara inatoa wito kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii kuupotosha umma kwa taarifa ambazo siyo sahihi na ambazo zinaleta usumbufu kwa watu wengine.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kutokana na kusambaa kwa taarifa hizo ambazo siyo za kweli.

Imetolewa na:

Dk. Leonard D. Akwilap

Katibu Mkuu

 

Read 10469 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…