Monday, 24 April 2017 08:08

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, AWAASA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya sekondari ya wasichana Kondoa kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo hayana tija kwa maisha yao.
 
Waziri Ndalichako amesema hayo wakati wa mahafali ya kidato cha sita shuleni hapo kuwa , mitihani siyo muujiiza na kuwa mitihani ya ndani ya shule huwa ni migumu tofauti na ile inayotoka nje ya shule kama vile mtihani wa taifa na mara zote maswali yanayoulizwa ni yale yale ambayo tayari mwanafunzi anakuwa amejifunza darasani.
 
 Waziri Ndalichako amewaasa wanafunzi hao kuhakikisha wanatumia uhuru wa vyuoni vizuri pindi watakapochaguliwa kujiunga na vyuo  kwani wanapokuwa chuoni hakuna ulinzi au usimamizi kama ule wa kwenye shule za msingi na zile za sekondari.
 
"Napenda kuwasihi sana wanangu kuwa mnapokaribia kumaliza elimu yenu hii ya sekondari na kwenda kujumuika na jamii nendeni mkaendeleze nidhamu na matendo mema ambayo walimu wenu wamewafundisha hapa shuleni, msiende kujiingiza kwenye majanga ya ukimwi, dawa za kuevya sitegemei muende mkapotoke, kuweni wazalendo na muwe mabalozi wazuri wa kuisemea nchi yenu."alisema Profesa Ndalichako.
 
Waziri Ndalichako amesema katika kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia na yale ya kujifundishia  tayari wizara imeanza Kusambza vitabu mashuleni, vifaa vya maabara, na vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. 
 
kwa upande wake Mlkuu wa  shule hiyo Flora Nusu amemweleza waziri baadhi ya changamoto  zinazoikabili shule hiyo kuwa ni Upungufu wa  walimu wa masomo ya sayansi ikiwemo Fizikia, Kemia, Biolojia, Hisabati,Pia Ukosefu wa ukumbi wa mikutano, uchakavu wa miundombinu ya maji kwa ajili ya vyoo, uchakavu wa nyumba za walimu, Ukosefu wa  Kompyuta kwa ajili ya kujifundishia.
Read 6477 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…