Thursday, 07 January 2021 23:27

TAARIFA KWA UMMA: MWALIKO KUSHIRIKI KIKAO CHA WADAU KUJADILI RASIMU YA MIONGOZO YA USALAMA WA MAZINGIRA NA JAMII KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUBORESHA ELIMU YA JUU KWA MABADILIKO YA KIUCHUMI (HEET) NCHINI

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, inafanya maandalizi ya kutekeleza Mradi wa Kuboresha Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation - HEET) Nchini.

Lengo la Mradi ni kuongeza udahili katika vyuo vikuu vya serikali, kuongeza ubora wa mafunzo ili kuendana na soko la ajira kwenye programu za kipaumbele na kuboresha utendaji wa Serikali katika kusimamia Elimu ya Juu nchini.

Utekelezaji wa mradi utazingatia miongozo ya usalama wa mazingira na jamii. Hivyo, WyEST imeandaa vikao vya wadau kwa ajili ya kupokea maoni ya wadau ili kuboresha rasimu ya miongozo mitatu (3) iliyoandaliwa. Miongozo hiyo ni Mwongozo wa Usimamizi wa Usalama wa Mazingira na Jamii (Environmental and Social Management Framework – ESMF), Mwongozo wa Uhamishaji wa Makazi na Watu (Resettlement Policy Framework - RPF) na Mpango wa Ushirikishwaji wa Wadau (Stakeholders’ Engagement Plan –SEP).

Vikao vya kupokea maoni ya wadau vitafanyika mkoani Dar es Salaam, kuanzia saa 9:00 asubuhi kwa kulingana na jedwali lifuatalo.

Wadau Ukumbi Tarehe
Taasisi zinazotekeleza Mradi wa HEET, Taasisi na wakala wa Serikali, Jumuiya za wataaluma vyuoni, Jumuisha za Wanafunzi Vyuoni, Jumuiya za wanafunzi wenye mahitaji maalumu Maktaba UDSM 13 Januari 2021
Asasi zisizo za Serikali, Mashirika, Makampuni, watu binafsi na wadau wa maendeleo Maktaba UDSM 14 Januari 2021

Kwa kuzingatia umuhimu wa miongozo hiyo, WyEST inawaalika wadau wote kufika na kutoa maoni yao kabla miongozo hiyo haijapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Baruapepe kwa anuani ifuatayo kabla ya tarehe
15 Januari 2021:-

Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
S.L.P. 10,
DODOMA
Baruapepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Aione: Tabitha Etutu

Miongozo hiyo pia inapatikana kupitia tovuti ya WyEST www.moe.go.tz

Read 277 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…