Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwa Mkurugenzj wa Mafunzo ya Ufundi Wizara ya Elimu, Dkt. Noel Mbonde na Mkurugenzi wa KTO ndugu Maggid Mjengwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za KTO, jijini Dar es Salaam.
Vitabu vilivyokabidhiwa ni vya kiada na ziada vitakavyotumika Kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 41 kati ya 55 nchini.
Vyuo hivyo ambavyo vipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia vinaendesha programu ya Elimu Haina Mwisho. Programu hii inawalenga vijana wa kike waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwamo za kiuchumi na Kijamii kupitia programu ya Elimu Haina Mwisho.
KTO imekuwa mdau mkuwa katika kuwezesha Vijana wanapata Elimu kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kwa kufadhil wanafunzi kupata mafunzo kupitia Programu hiyo ya Elimu Haina Mwisho.
Wanawake Vijana wanaojiunga na Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi hupata elimu ya Sekondari na ufundi kwa miaka miwili na kisha kuendelea na Masomo katika Mfumo Rasmi baada ya kufaulu mitihani.
Vitabu hivyo vimetolewa kwa ufadhili wa nchi ya Sweden na Taasisi ya Mastercard Foundation yenye makao yake nchini Canada.