Thursday, 05 March 2020 00:05

MAKTABA MPYA YAZINDULIWA CHUO CHA UALIMU KOROGWE

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Machi 5, 2020 amezindua maktaba mpya ya Chuo cha Ualimu Korogwe kilichopo Mkoani Tanga.

Akizungumza na baadhi ya walimu tarajali na wanafunzi aliowakuta katika maktaba hiyo mara baada ya kuizindua Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao kuitumia vyema maktaba hiyo kwa lengo la kujipatia maarifa na kuongeza uwezo katika taaluma.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akimkaribisha Waziri Mkuu amesema
Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 338 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maktaba hiyo ambayo ujenzi wake ukianza kwa Micjango ya Wananchi wa Korogwe.

Katibu Mkuu huyo amesema Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuunga mkono juhudi za wananchi ambao walichanga shilingi milioni 1.9 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.

"Wananchi wa Korogwe waliona umuhimu wa chuo hiki kuwa na maktaba na wakaanza kuchanga fedha na kuanza ujenzi" amesema Dkt. Akwilapo.

Mmoja wa walimu tarajali katika Chuo cha Ualimu Korogwe Emanuela Bombo ameishukuru Serikali kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa maktaba hiyo kwani itasaidia katika ujifunzaji.

Maktaba hiyo ina vifaa vya kisasa pamoja zikiwemo kompyuta ambazo zinawezesha matumizi maktaba mtandao na kwamba Maktana itatumiwa na walimu tarajali zaidi ya 1000 ambao wanasoma masomo ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA na pia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wa wilaya ya Korogwe.

Read 1230 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…