|
>>Kuhusu Maendeleo ya Utamudini |>> Baraza la Sanaa |>>Baraza la Kiswahili (Kiswahili) (English) | >>Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza >>| Machapisho Muhimu|>>Mapromota
Maendeleo ya Utamaduni
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ina wajibu wa kuongoza, kusimamia, na kudhibiti shughuli za ukuzaji wa Sanaa za Maonyesho, Ufundi na Muziki; kusimamia ukuzaji wa lugha ya Kiswahili, lugha za Asili na za Kigeni; na kusimamia shughuli za Mila na Desturi.
Majukumu ya Idara
- Kuandaa mipango ya ukuzaji lugha, sanaa, maadili na utafiti wa mila na desturi.
- Kukusanya, kuhifadhi na kusambaza takwimu muhimu za utamaduni ili kufanikisha shughuli za utamaduni za utawala, uendeshaji, mipango na biashara.
- Kuratibu maonyesho, mashindano na matamasha ya utamaduni kitaifa na kimataifa.
- Kukuza matumizi ya lugha sanifu, fasaha pamoja na uandishi.
- Kuratibu shughuli za ushirikiano wa utamaduni baina ya Tanzania na nchi nyingine na katika mashirika ya kimataifa kama vile UNESCO, SADC, EAC na EACROTANAL.
- Kusimamia utendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Baraza la Sanaa la Taifa, Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Chuo cha Sanaa, Bagamoyo.
Back top
Baraza la Sanaa
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1984. BASATA hujishughulisha na kuhimiza maendeleo ya sanaa zifuatazo: Muziki, Maonyesho na Ufundi wa Mikono. Shughili hizo hufanywa na wananchi, wengi wakiwa katika vikundi, vyama, makampuni na hata wasanii binafsi. Mara nyingi uzalishaji wa sanaa hutegemea vipaji binafsi vya wasanii na nyenzo rahisi na nyepesi.
MAJUKUMU YA BASATA
-
Kubeba dhamana ya kufufua na kukuza maendeleo na kuongeza uzalishaji wa kazi za sanaa ikiwa ni pamoja na utumiaji wa vyombo vya muziki, nyimbo, mashairi na ngoma za asili za mapokeo ili kuendeleza utumaduni wa Tanzania.
-
Kufanya Utafiti wa maendeleo ya uzalishaji wa kazi za sanaa na utafutaji wa masoko ya kazi hizo ikiwa ni pamloja na kufanya Utafiti wa viwango na thamani ya kazi za sanaa zinazofanywa Tanzania.
-
Kutoa huduma za ushauri na misaada ya kiufundi ambayo ni ya lazima au ya nyongeza katika kuendeleza shughuli za sanaa kwa mashirika ya umma na kwa watu mbalimbali wanaojishughulisha na kazi hizi.
-
Kuandaa mipango na kuratibu shughuli za sanaa zinazofanywa na watu mbalimbali Tanzania.
-
Kuishauri serikali juu ya mambo yahusuyo maendeleo ya uzalishaji wa kazi za sanaa nchini Tanzania.
-
Kuhimiza maendeleo ya kazi za sanaa kwa kuandaa na kufanya maonyesho, kucheza ngoma, kuendesha warsha, semina na mashindano baina ya wasanii mbalimbali.
-
Kuandaa sheria ndogo zitakazochapishwa katika Jarida na kuthibitisha mfumo wa usajili na watu wanaojipatia kipato kutokana na kucheza muziki, kutengeneza zana za muziki, kurekodi kwenye santuri au kanda kwa ajili ya matumizi au wanaojishughuyllisha na jambo la namna yoyote ambalo linahusiana na muziki wa namna iwayo yoyote ile.
Back top
Baraza la Kiswahili la Taifa
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho kwa sheria namba 7 ya mwaka 1983. Kama chombo cha serikali, lina dhamana ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.
MAJUKUMU YA BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA
-
Kustawisha maendeleo ya utumiaji wa Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
-
Kushirikiana na vikundi vingine ili kukiwezesha Kiswahili kutumika katika nyanja mbalimbali za utoaji wa elimu (kusanifu istilahi za taaluma mbalimbali).
-
Kutoa idhibati ya vitabu vya kiada vitakavyotungwa au kufasiriwa kwa Kiswahili kwa mahitaji na matumizi ya shule na kwa watu binafsi.
-
Kusimamia na kufuatilia Kiswahili fasaha katika vyombo vya habari (magazeti, TV, redio, n.k.)
Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza
Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza iliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 4 ya 1976.
MAJUKUMU
Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza itafanya kazi zifuatazo
-
Kuhakikisha kwamba Filamu na Michezo ya Kuigiza inawajibika na kuwiana na kawaida, milla, dessturi na maadili mema ya Tanzania;
-
Kuhakikisha kwamba Filamu na Michezo ya Kuigiza inatoa burudani yenye mafunzo mema na safi kwa Watanzania;
-
Kuhakikisha kwamba upangaji wa madaraja ya maonyesho ya filamu na michezo ya kuigiza unalingana na mabadiliko ya maadili mema ya jamii ya Watanzania;
-
Kuhakikisha kwamba usanii na uhuru wa ubunifu wa sanaa hauzuiliwwi bila sababu za msingi;
-
Kuhakikisha kwamba Filamu na Michezo ya Kuigiza, nchini Tanzania, inakuwa na viwango vinavyosstahili vy a ujumi na usanii;
-
Kuafiki, kuzuia au kudhibiti maonyesho na usambazaji wa filamu na michezo ya kuigiza;
-
Kuamuru kuondolewa kutoka kwenye filamu au mchezo wa kuigiza uliowasilishwa kwenye Bodi Kuu ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza sehemu yoyote ambayo Bodi Kuu haiiafiki kwa maonyesho au usambazaji kwa Watanzania;
-
Kuafiki, kuzuia au kudhibiti utangazaji kwa umma unaohusiana na filamu au michezo ya kuigiza;
-
Kukagua na kupanga madaraja ya filamu na michezo ya kuigiza.
-
Kukagua na kutoa vibali kwa maeneo yote yanayotumika kwa maonyesho na usambazaji wa filamu au michezo ya kuigiza.
-
Kuafiki na kutoa vibali kwa shughuli za usambazaji wa filamu na michezo ya kuigiza
-
Kuafiki na kutoa vibali kwa maonyesho ya filamu na michezo ya kuigiza.
Back top
Arts Training Institutions
Shule, Vyuo na Taasisi za Mafunzo
Katika miaka ya 1970 na 1980 taasisi za mafunzo ya sanaa za Butimba na Bagamoyo zilianzishwa.
Arts Training Institutions
Arts training institutions in Butimba and Bagamoyo were created in the seventies and eighties respectively.
Chuo Cha Ualimu Butimba
Programu ya mafunzo ya sanaa ya Chuo cha Ualimu Butimba ilikusudiwa mahususi kulenga katika kuwapata walimu wa sanaa kwa ajili ya shule za msingi na sekondari.
Kwa habari zaidi angalia tovuti
Butimba Teachers Training
The Butimba Teacher Training arts training programme was aimed specifically for producing arts teachers for primary and secondary schools.
For further information see link website……..
Chuo cha Sanaa Bagamoyo
Chuo cha Sanaa Bagamoyo ilikusudiwa mahususi kuwafunza wahamasishaji na mameneja wa sanaa kwa ajili ya maendeleo ya sanaa kwa jumla nchini.
Kwa habari zaidi angalia tovuti www.sanaabagamoyo.com
Bagamoyo College of Arts
The Bagamoyo College of Arts was aimed at producing arts animators and managers for the general public arts development of the country.
For further information, see link website www.sanaabagamoyo.com
Machapisho Muhimu
:::: Cultral Development Policy
:::: Culture Development Master Plan 
:::: Mapromota 
:::: Matamasha
ya Utamaduni 
:::: Wasanii Maarufu

:::: Waliotunukiwa Tuzo ya Zeze 1999 - 2004
|