EDUCATION DEPARTMENTS --chief education officer


>>introduction |>> Registration of schools and teachers |>> special education| >>Adult and Non-formal Education |>>Education by Radio| >>Environmental Education >>Guidance and counseling HIV Aids

Environmental Education

UTANGULIZI

Sehemu ya Elimu ya Mazingira katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilianzishwa mwaka 2001 chini ya ofisi ya Afisa Elimu Kiongozi.

Sehemu hii inaratibu ufundishaji na kujifunza Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu katika shule za Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo ya Ualimu, Ufundi na Elimu ya Watu Wazima.

Mafunzo haya ya Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.ni muhimu katika shule, vyuo na watu wazima ili kusaidia kuboresha mazingira ya shule na jamii kwa ujumla.

 

MAJUKUMU

  1. Kubuni mikakati inayolenga kuboresha ufundishaji na kujifunza Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu katika Shule, Vyuo  na Elimu ya watu Wazima.
  2. Kushiriki katika mchakato wa kurekebisha mtaala unaotumika kufundishia shuleni, vyuo na Elimu ya Watu Wazima kwa lengo la kuingiza mada za Elimu ya Mazingira katika masomo yote  na shughuli za uzalishaji mali.
  3. Kuhamasisha uingizaji wa dhana ya Elimu ya Mazingira katika ufundishaji na kujifunza masomo yote katika shule, vyuo na elimu ya watu wazima kwa kuhakikisha kuwa dhana ya Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu inaingizwa katika shughuli na mipango yote ya maendeleo ya watu wazima.
  4. Kuhamasisha walimu kuongoza wanafunzi kufanya tafiti za kimazingira ili kubaini hali ilivyo na kutoa ushauri kwa vyombo vinavyohusika kwa kutumia mkakati wa ‘GLOBE Programu’.
  5. Kuandaa sera inayolenga kuinua ubora katika ufundishaji na kujifunza Elimu ya Mazingira na Elimu kwa Maendeleo Endelevu  katika ngazi zote.
  6. Kuidhinisha miradi ya uboreshaji wa mazingira inayoweza kufanyika shuleni na vyuoni.
  7. Kuratibu, kutayarisha na kushiriki katika mikutano, warsha na makongamano yanayolenga kuboresha Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu katika shule,vyuo na jamii.
  8. Kushiriki katika utayarishaji wa vipindi/makala za Elimu ya Mazingira katika radio, televisheni, magazeti n.k
  9. Kuwa kiungo kati ya Wizara na Mashirika mbali mbali ya nje na ndani ya nchi yanayoshughulikia Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.
  10. Kubainisha vifaa vinavyohusiana na Ufundishaji wa Elimu ya Mazingira na kushiriki katika kutayarisha makala mbalimbali.
  11. Kutoa ushauri mbalimbali wa kitaalamu kuhusu Elimu ya Uhifadhi wa Mazingira katika shule, vyuo na jamii.
  12. Kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji na kujifunza Elimu ya Mazingira katika shule, vyuo na elimu ya watu wazima.

 

MAFANIKIO

  1. Nakala 150,000 za Kishwahili za Mwongozo wa Kufundishia Elimu ya Mazingira kwa shule za msingi zimetolewa na kusambazwa katika shule zote za msingi hapa nchini. Nakala 5,000 za Kiingereza za Mwongozo huu zilitolewa na kusambazwa katika nchi zilizoko katika Bonde la Mto Nile. Nakala zaidi zinahitajika kuchapishwa ili kukidhi mahitaji.
  2. Walimu na wakaguzi 810 wa shule za msingi wa kanda ya mashariki (400), kati (50), kaskazini mashariki (50), kaskzini magharibi (50), kusini (50) na ADEM (160) wamepatiwa mafunzo ya uelimishaji wa jinsi ya kuingiza dhana ya mazingira na kufanya tafiti katika mazingira.
  3. Rasimu za vitini vya kufundishia Elimu ya Mazingira katika somo la Stadi za Kazi kwa shule za msingi zimetolewa.
  4. Warsha zimeendeshwa kwa ajili ya kuwawezesha walimu, wakaguzi wa shule, wakuza mitaala, pamoja na wadau wengine wa Elimu ya Mazingira kuhusu ujanishaji shule [Eco – Schools Approach] na jinsi ya kufanya utafiti katika mazingira [GLOBE Program].
  5. Rasimu ya Tatu ya Mkakati wa kufundishia Elimu ya Mazingira kwa shule na vyuo imetolewa na kusambazwa kwa wadau ili kutoa maoni yao.
  6. Warsha 02 za wadau mbali mbali zimeendeshwa kwa ajili ya uzinduzi wa hatua za utekelezaji wa mpango wa kufundisha Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.

 

MATARAJIO

    • Kutayarisha Mwongozo wa kufundishia Elimu ya Mazingira kwa shule za sekondari, vyuo na watu wazima.
    • Kufanya na kuhamasisha shule na vyuo kufanya utafiti katika mazingira, Elimu ya Mazingira na uhifadhi wa mazingira ili kubaini hali iliyopo na kuweka mikakati ya uboreshaji wa Elimu ya Mazingira kwa Maendeleo Endelevu katika jamii.
    • Kutayarisha na kushiriki katika mikutano, semina, warsha na makongamano yanayolenga kuboresha Elimu ya Mazingira katika shule,vyuo na elimu ya watu wazima ili kukuza uelewa.
    • Kutoa mafunzo kwa waelimishaji walimu na wakaguzi wa shule za msingi ili nao waweze kuwaelimisha wenzao jinsi ya kuingiza dhana ya mazingira na kufanya tafiti katika mazingira kwa kanda ya nyanda za juu, magharibi na ziwa.

    Back top

   
Tanzania Government Website | National Examination Council | Tanzania Online | Search Engines |
Ministry of Education and Vocation Training © 2005 All rights reserved