Mihtasari Mipya ya Mafunzo ya Ualimu - 2009
Mihtasari ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada imeboreshwa na kuidhinishwa kuanza kutumika rasmi kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010. Utekelezaji wa mihtasari hii uzingatie maelekezo ya Kamishna wa Elimu kuhusu ufundishaji na utahini wa mihtasari hii kuanzia Septemba 2009. Mihtasari hii ni kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali na Visivyo vya Serikali. Utekelezaji wa Mihtasari ya Elimu kwa Michezo na Elimu ya Awali utatolewa maelekezo rasmi na wizara.